Na.DevothaSongorwa,Morogoro ..........................................................................................................................
Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro limewataka wananchi kutii sheria za nchi bila shuruti ili kulinda amani ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro ACP LEONCE RWEGASIRA amesema hayo kufuatia Operesheni UKUTA inayotarajia kufanyika mapema mwezi ujao ikiongozwa na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Kamanda RWEGASIRA amesema Jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kusimamia sheria na wote watakaokiuka sheria watachukuliwa hatua za kisheria bila kujali wadhifa wao.
Aidha amewataka wananchi kuacha kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo rasmi na badala yake wafuate taratibu ili kuepukana na vurugu na uvunjifu wa amani.
Home
News
Slider
OPERESHENI UKUTA:Polisi Morogoro yatahadharisha wananchi kutii sheria bila Shuruti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment