KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm, amewaomba mashabiki wa timu
hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo wao wa marudio wa Kombe la
Shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria, unaotarajiwa kuchezwa
Jumamosi Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Yanga itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa
awali kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao hao, katika mchezo wa
kwanza wa Kundi A.
Pluijm alisema ni wakati wa mashabiki
wa timu hiyo kuendelea kuwasapoti na kuwaamini ili kuweza kufanya vizuri
katika michezo yao iliyobakia ukiwamo wa Mo Bejaia.
“Kwani wiki hii wachezaji wameonekana kuwa na ari na hamasa ya
kujituma uwanjani, inatupa faraja najua sitakuwa na mshambuliaji wangu,
Donald Ngoma, aliyekuwa na kadi mbili za njano, Nadir Haroub (Cannavaro)
kutokana na kuwa na majeruhi ya kifundo cha mguu lakini haitanifanya
nikate tamaa,” alisema Pluijm.
Naye nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘ Cannavaro’ , amesema
watatengeneza ukuta imara ili kutoruhusu mabao katika mchezo wao wa
kesho.
Cannavaro amesema kuwa beki ya Yanga ikiongozwa
na yeye mwenyewe wataweka ukuta imara kuhakikisha washambuliaji wa Mo
Bejaia hawaleti madhara.
“Moja ya safu ambazo kama hazijipangi vema zinaweza kuiletea madhara
timu ni ngome ya ulinzi, sasa tutahakikisha kwamba hapiti mtu,” alisema
Cannavaro. Naye mshambuliaji Mrundi, AmissiTambwe, ametamba kuwa lazima
afunge katika mchezo huo baada ya kukosa bahati ya kufunga katika
michezo iliyopita.
“Nimeshawasoma wapinzani tangu mchezo ule wa kwanza, hivyo nawatambua
na kamwe hawatanibabaisha nitahakikisha napambana kufa au kupona,”
alisema Tambwe. Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini
Ethiopia ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Bamlak Tessema Weyesa,
akisaidiana na Kindie Mussioe na Temesgin Samuel Atango na mwamuzi wa
akiba akiwa ni Haileyesus Bezezew Belete.
Viingilio vya mchezo huo vitakuwa ni Sh 3,000 kwa viti vya rangi ya
kijani, bluu na chungwa, VIP B na C vikiwa ni Sh 10,000 huku VIP A ni Sh
15,000. Katika kundi hilo Yanga inashika mkia kwa kuwa na pointi moja,
wakati mpinzani wake Mo Bejaia ikiwa nafasi ya pili kwa pointi sita,
nafasi ya tatu Medeama ya Ghana yenye pointi nne huku kinara TP Mazembe
ikiwa na pointi saba.
Home
MICHEZO
Slider
Pluijm awaomba mashabiki kujitokeza kwenye mchezo wa Yanga Vs Mo Bejaia ya Algeria jumamosi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment