Muungano wa wafanyakazi nchini Sudan SWTUF,
umeandaa maandamano katika mji mkuu wa Khartoum kwa ajili ya kupinga
jaribio la mapinduzi ya FETO na kuunga mkono serikali ya Uturuki.Maandamano
hayo yalihudhuriwa na balozi wa Uturuki mjini Khartoum Cemalettin
Aydın, msimamizi wa Memur-Sen Ali Yalçın, mkuu wa HAK-İŞ Mahmut Arslan
pamoja na mamia ya raia wa Sudan.
Waandamanaji walibeba bendera za Kituruki na kuonyesha msimamo wao wa pamoja na serikali ya Uturuki.
Wananchi wa Sudan waliipongeza serikali ya Uturuki na wananchi wake kwa ujasiri wa kujitoa mhanga kuzuia jaribio la mapinduzi.
Balozi Aydın alitoa maelezo kwa waandishi wa habari na kutangaza kufuatilia makini suala la kuweka usimamizi mpya wa shule za FETO nchini Sudan.
Aydın aliongezea kusema kuwa viongozi kutoka wizara ya elimu ya Uturuki pia itaweza kutekeleza ziara ya Sudan katika siku zijazo.
Sudan ni mojawapo ya nchi zilizopinga jaribio la mapinduzi ya FETO na kuunga mkono serikali ya Uturuki kwa kuchukuwa hatua ya kusitisha uendeshaji wa shule za kundi hilo.

0 comments:
Post a Comment