Leo
Agosti 11/2016 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape
Moses Nnauye amelifungia gazeti la Mseto kwa miezi 36 mara baada ya ya
kuandika habari zenye kumchafua Naibu waziri Ngonyani.
Siku chache
zilizopita waziri Nape alitahadharisha vyombo vya habari kuandika habari
zenye tija kwa jamii na kwa taifa zima,huku akisema kuwa kwa chombo
kitakacho ripoti taarifa za maandamano,mikutano kwa uchochezi kamwe hata
vifumbia macho kwakuwa vinahamasisha uchochezi unaoweza kuogofya jamii.
Waziri
nape katika tahadhari yake alisema kuwa vyombo vya habari visiwe chanzo
cha kuchonganisha serikali na wananchi kwa kuandika habari za
kichochezi na kuacha habari zenye tija kwa taifa na zenye kuletea tafa
maendeleo.
Gazeti la Mseto ambalo lilichukua nafasi ya Mwanahalisi
katika uandishi wake wa habari za uchunguzi zinazoandikwa kwa mfumo wa
makala nisiku moja tu hadi hivi leo ambapo 10 Agosti 2016 Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Edwin A. Ngonyani alilitaka
gazeti hilo la la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilingi
bilioni moja kutokana na kuandika habari ya kumchafua.
Jana
akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake Waziri Ngonyani alisema
kuwa Gazeti hilo la tarehe 4 Agosti 2016 liliandika habari yenye kichwa
cha Habari “Waziri amchafua JPM” ikimuhusisha na upokeaji wa fedha
kutoka moja ya Kampuni ya Madini wakati akiwa Kaimu Mkurugenzi wa
Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
“Nimewaandikia notisi ya siku
saba ikiwataka waombe radhi na kunilipa fidia, na wasipofanya hivyo
hatua stahiki kuwapeleka mahakamani akiwemo Mwandishi Josephat Isango,
Mwanahalishi Publisher na Mchapaji wa gazeti hilo”. Alisema Mhandisi
Ngonyani.
Mhandisi Ngonyani alisema kuwa habari hiyo siyo ya kweli na
mwandishi ametumia nyaraka za kughushi ikiwemo barua iliyoandikwa
tarehe 24 Julai na kutiwa saini yake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO
wakati ukweli ni kwamba tarehe hiyo yeye alikuwa ni Mkurugenzi kamili na
siyo Kaimu kama barua hiyo inavyosomeka.
Aliongeza kuwa habari hiyo
imewachafua watu wengi ikiwemo familia yake, wapiga kura wake wa jimbo
la Namtumbo ambao walijitoa katika kumsaidia wakati wa kampeni na hali
kadhalika zimemchafua Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumhusisha
na fedha kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwaahidi kuwa mitaji yao
nchini itakuwa salama.
“Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli alishasema kama
kuna mfanyabiashara yeyote aliyechangia kuingia kwake ikulu ajitokeze
na hakuna aliyefanya hivyo, Iweje leo mtu tu anaibuka na kuandika habari
za kugushi? ”. Aliongeza.
Aidha Naibu Waziri huyo alitumia fursa
hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa waangalifu pindi
wanapoandika habari za kutunga kwa kutotumia majina halisi kwani kufanya
hivyo ni kwenda kinyume na kanuni za uandishi wa hadithi (Habari za
kutunga).
“Waandishi wa habari mnatakiwa kufuata maadili ya kazi yenu
kwa kuandika habari zenye ukweli ili kuliepusha taifa kuingia katika
machafuko na migogoro isiyo ya lazima” Alisema Naibu waziri huyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment