Image
Image

Idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye shambulizi la kigaidi lililotekelezwa Libya yafikia 19

Idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye shambulizi la kigaidi lililotekelezwa na DAESH mjini Sirte nchini Libya imeripotiwa kufikia 19.Idadi ya majeruhi wa shambulizi hilo lililotekelezwa kwa kutumia mabomu yaliyotegwa ndani ya magari mawili pia inaarifiwa kufikia 80.
Baada ya shambulizi hilo, ndege za vikosi vya Marekani zilianzisha operesheni za angani dhidi ya DAESH.
Mnamo mwezi Mei, serikali ya maridhiano nchini Libya ilitangaza kuanzisha operesheni dhidi ya ugaidi inayotambulika kama ‘Al-Bunyan al-Mersus.’
Wakati wa operesheni hiyo, ngome nyingi za magaidi ziliweza kutekwa na kuanza kudhibitiwa na vikosi vya usalama.
Vyanzo vya usalama vimetoa taarifa ya uwezekano wa kusafishwa na kuangamizwa kwa kundi la DAESH kikamilifu kwenye operesheni za Marekani ndani ya muda mfupi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment