Serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza Alhamisi hii, Agosti 18,
amri ya kutotoka nje usiku katika miji ya Beni na Butembo, mashariki
mwa nchi hiyo, baada ya maandamanoya Jumatano wiki hii dhidi ya
serikali.
Wakazi wa miji hiyo wametakiwa kutotoka nje kuanzia saa
moja usiku gadi saa kumi na mbili asubuhi. Tangazo hili limetolewa na
Naibu Waziri Mkuu mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani, Evariste Boshab.
Hatua ambayo haikuwaridhisha wafanyabiashara. Wafanyabiasha katika mji
wa Beni waliamua Alhamisi hii kufunga maduka yao katika barabara kuu ya
Nyamwisi. Wafanyabiashara wanaomba kuachiwa huru kwa waandamanaji
wanaozuiliwa.
Katikati mwa mji wa Beni, maduka yalifungwa Alhamisi
hii Agosti 18 kwenye barabara kuu ya Nyamwisi ambapo ni moja ya meneo
kulikofanyika maandamano ya Jumatano. Wafanyabiashara wameeleza kwamba
bado wanaomboleza wahanga wa tukio hilo. kuu wa mji wa Beni alisema kuwa
mtu mmoja ndio aliyeuawa kwa risasi na askari polisi aliyeuawa kwa
kupigwa mawe. Mtu mwengine aliuawa katika maandamano hayo, idadi hii ni
kubwa mwa raia, amesema mmoja wa wafanyabiashara.
Wafanyabiasaha
wanadai pia kuachiwa huru kwa waandamanaji wote na kurejeshwa kwa vifaa
vya viliyopokonywa na vikosi vya usalama. Hatutofungua maduka kama madai
yetu hayatopatiwa ufunbuzi, amesema mfanyabiashara mmoja. Mfanyabiasha
mwingine amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna uwezekano raia
kuingia tena mitaani.
Kabla ya kuondoka, Naibu Waziri Mkuu mwenye
dhamana ya Mambo ya Ndani alisema kuwa watu waliokamatwa watahojiwa na
kisha waachiliwe. Evariste Boshab alisema alipewa taarifa ya watu saba
waliokamatwa. Lakini asasi za kiraia, zinasema kuwa zina idadi ya
waandamanaji 148 wanaozuiliwa, ikiwa ni pamoja na watoto 15 na wanawake
36.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment