Na.DevothaSongorwa,Morogoro
...............................................................................................................................
Serikali
mkoani Morogoro imesema inaendelea na shughuli za ujenzi na uboreshaji
viwanda ili kutimiza ahadi iliyotolewa wakati wa kampeni na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. JOHN POMBE MAGUFULI kuifanya nchi
kuwa ya viwanda.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk. KEBWE
STEPHEN KEBWE wakati akizungumza na wananchi kwenye uwanja wa jamhuri
ambapo amesema kuwa serikali imetenga eneo la Mkonge lililopo Tungi
kujengwa viwanda na makazi.
Ameongeza kuwa maeneo ya Mazava serikali
inatarajia kujenga kiwanda kitakachochakata nguo za michezo na
wanatarajia kutoa ajira kwa zaidi ya watu 7000, ili kupunguza janga la
umaskini, ukosefu wa ajira na kuliongezea pato taifa.
Aidha Mkuu
wa mkoa huyo Dk. KEBWE amesema serikali ina mpango wa kuendeleza kilimo
kuwa chenye tija, kumaliza ujenzi wa shule za sekondari, maabara,
zahanati na nyumba za walimu, matumizi bora ya ardhi kwa taifa ili
kumaliza mgogoro uliopo kwenye wilaya mbalimbali ikiwemo Mvomero,
Kilombero, Malinyi, na Ulanga pamoja na kusimamia uhifadhi wa vyanzo vya
maji kuepukana na changamoto ya maji mkoani Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment