Idara
mbalimbali za serikali katika Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,
zimeanza kutekeleza maelekezo ya serikali zao kuanza kupeperusha Bendera
ya Jumuiya hiyo sambamba na ile ya taifa katika Ofisi zao.
Mbali na
Bendera, wimbo wa Jumuiya hiyo umetakiwa kuimbwa katika shughuli zote za
kitaifa, pindi tu baada ya ule wa taifa husika.
Jumuiya ya Afrika
Mashariki ina mataifa matano; Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi
na Sudan Kusini ambayo ilijiunga mwaka huu
Bendera na wimbo wa taifa
wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni nembo muhimu zinazoonesha umoja wa
watu wa Afrika Mashariki kuelekea kwenye shirikisho la kisiasa katika
siku zijazo.
Mwisho wa mwezi uliopita, serikali ya Kenya iliagiza
bendera ya Jumuiya kupeperushwa sambamba na ile ye taifa na wimbo wa
Jumuiya kuchezwa katika shughuli zote za kitaifa.
Agizo kama hili
lilitolewa nchini Tanzania na limeanza kutekelezwa sawa na Uganda ambayo
imekuwa katika mstari wa mbele kutekeleza hili kwa muda mrefu sasa.
Wana Afrika Mashariki wamekuwa wakihimizwa kuufahamu wimbo wa Jumuiya;
WIMBO WA JUMUIYA
Kiitikio
Jumuiya Yetu sote tuilinde
Tuwajibike tuimarike
Umoja wetu ni nguzo yetu
Idumu Jumuiya yetu.
Stanza
1.Ee Mungu twaomba ulinde
Jumuiya Afrika Mashariki
Tuwezeshe kuishi kwa amani
Tutimize na malengo yetu.
2.Uzalendo pia mshikamano
Viwe msingi wa Umoja wetu
Natulinde Uhuru na Amani
Mila zetu na desturi zetu.
3.Viwandani na hata mashambani
Tufanye kazi sote kwa makini
Tujitoe kwa hali na mali
Tuijenge Jumuiya bora.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment