Image
Image

Jaribio la Chanjo ya Zika kwa Tumbili lafaulu Marekani.

Majaribio matatu ya chanjo kwa mnyama aina ya Tumbili yameonyesha kuzaa matunda .
Majaribio hayo ya chanjo hiyo yalifanyiwa kwa Tumbili watatu na mtaalamu wa afya Dk Dan Barouch  katika kituo cha afya cha Beth Israel Deaconess  kilichoko nchini Marekani.
Ripoti ya matokeo ya chanjo hiyo ilitolewa katika jarida la sayansi na kufahamisha kuwa chanjo hiyo itaweza kutumika kwa binadamu mwaka 2017.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa ni kwamba raia zaidi ya 650,000 kutoka Marekani waliokuwa wanasafiri kwenda mataifa mengine walipatikana na virusi hivyo vya Zika .
Shirika la Afya la Dunia (WHO)pia lilitoa ripoti mnamo Julai 27 iliyoonyesha kuwa virusi vya Zika vilipatikana  katika mataifa 67 .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment