Msemaji
wa ikulu ya nchi hiyo Manoah Esipisu amesema, hatua hiyo imekuja baada
ya mazungumzo kati ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na ujumbe wa Sudan
Kusini uliokuwa ziarani nchini Kenya, na kusema lengo la mkutano huo
lilikuwa ni kuomba msaada wa Kenya.
Wakati
huohuo, China imeahidi kutoa dola za kimarekani milioni 10 ili
kuisaidia Sudan Kusini kukabiliana na mahitaji ya kibinadamu. Balozi wa
China nchini humo Ma Qiang amesema, fedha hizo zitatumika kununua
chakula na mahitaji mengine, ikiwa ni juhudi za kuokoa maisha ya maelfu
ya watu walio kwenye hali mbaya ya kibinadamu.
Habari
nyingine zinasema, makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Taban Deng,
amewasili nchini Sudan jana kwa ziara ya kiserikali. Deng alifanya
mazungumzo na makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Bakri Hassan Saleh hapo
jana, na hii leo anatarajiwa kukutana na rais Omar al-Bashir wa Sudan.


0 comments:
Post a Comment