SERENGETI Boys imebakisha kikwazo kimoja kabla ya kufuzu kucheza
fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17,
baada ya kuifunga Afrika Kusini 2-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex,
Mbagala jijini Dar es Salaam.
Baada ya ushindi huo wa jana, Serengeti Boys sasa itacheza na mshindi
wa mchezo wa Congo Brazzaville na Namibia kabla ya kufuzu kwa fainali
hizo zitakazofanyika Madagascar mwakani.
Serengeti Boys iliandika bao la kuongoza katika dakika ya 35
lililofungwa na Mohamed Abdallah baada ya kupata krosi ya Yohana
Mkomola. Muhsin Makame aliihakikishia ushindi Serengeti Boys pale
alipofunga bao la pili katika dakika ya 84 baada ya pasi nzuri ya
Mohamed Abdallah.
Serengeti Boys ilipata pigo pale mchezaji wake, Ally Ng’azi
alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Bonga
Dladla.
Awali, Serengeti Boys ndio ilikuwa ya kwanza kuliweka majaribuni
lango la wapinzani wao baada ya Mohamed Abdallah kushindwa kufunga
katika dakika ya tatu licha ya kuwa katika nafasi nzuri kwani alipiga
mpira nje.
Wenyeji nusura wafunge katika dakika ya 14 wakati Kelvin Naftal
alipokuwa katika nafasi nzuri lakini kabla hajaleta madhara, mabeki wa
Afrika Kusini waliokoa hatari hiyo.
Kocha wa Serengeti Bakari Shime `Mchawi Mweusi’ aliipongeza timu yake
kwa ushindi huo na kusema kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kuliko ule wa
awali, ambao timu hizo zilitoka sare ya kufungana 1-1 Afrika Kusini na
kuifanya kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.
Kikosi cha Serengeti Boys: Ally Msengi, Ramadhani Kabwili, Nickson
Job, Israel Mwenda, Ally Ng’azi, Kelvin Naftal, Shaban Ada, Mohamed
Abdallah, Yohana Mkomola na Asad Juma/Issa Makamba.
Home
MICHEZO
Slider
SERENGETI Boys imebakisha kikwazo kimoja kabla ya kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment