CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeendelea kushikilia
msimamo wa kuendeleza operesheni UKUTA Septemba mosi mwaka huu.
Rais John Magufuli alipiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa
isiyo na lengo jema ikiwemo ya viongozi kutoka kwenye maeneo yao kwenda
kufanya mikutano kwenye maeneo mengine, jambo linalopingwa na Chadema
kwa maelezo kuwa ni ukiukaji wa demokrasia.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, alisema kwenye Baraza la Mashauriano la
Kanda ya Pwani, lililofanyika jana Dar es Salaam kuwa wataitaarifu
Polisi kuhusu maandamano yao watakayoyafanya bila kubeba silaha ili
wapewe ulinzi.
Kwa mujibu wa Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa Kanda ya
Pwani, hawategemei kufanya fujo katika maandamano hayo, bali
watatekeleza wajibu wao wa kudai demokrasia ambayo ni haki yao ya
kikatiba, huku wakiwa wamejifunga vitambaa vyeupe mkononi na fulana
nyeusi.
“Atakayefanya fujo katika maandamano hayo hayo Polisi watakuwa na
haki ya kumkamata, vinginevyo tutadai haki yetu ya kidemokrasia ya
kufanya mikutano na shughuli za kisiasa kwa njia ya amani”, Mdee
alisema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment