Mkutano
Mkuu Maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), uliofanyika jana jijini Dar es
Salaam ukilenga kuwachagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa chama
hicho ulivunjika baada ya wajumbe kuanza kurushiana viti na matusi baada
ya kupishana katika hoja ya kumtosa aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa
Ibrahim Lipumba.
Profesa Lipumba alijiuzulu nafasi yake kabla ya
kampeni za uchaguzi Mkuu mwaka jana akieleza kuwa roho inamsuta kumnadi
mgombea urais aliyeungwa mkono na vyama vya Ukawa. Lakini mwaka huu
alirejea na kuandika barua akiomba kurejea kwenye nafasi yake hali
iliyozua sintofahamu.
Taarifa kutoka ndani ya Mkutano huo zimeeleza
kuwa wajumbe 832 walihudhuria lakini hoja ya kumjadili Profesa Lipumba
ilipofikiwa, baadhi ya wajumbe ambao wanamuunga Mwenyekiti huyo wa
zamani walizua vurugu wakipinga utaratibu uliotumika.
Baadhi ya
wajumbe hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa viongozi waliopo
madarakani walifanya ubabe kwa kulazimisha kura ya kukubali au kukataa
ombi la Lipumba ipigwe kwa uwazi na sio siri kama Katiba inavyoeleza.
“Haki
haikutendeka, ni ubabe. Wala mkutano haikuzingatia kutimia kwa akidi.
Tulilazimishwa kupiga kura kwa kunyoosha mikono wakati mazingira
yaliyopo na usahihi, kura ni siri,” mmoja wa wajumbe hao alikaririwa.
Baada
ya kupiga kura za wazi, Lipumba alipata kura 14 kati ya kura 832 hivyo
kuonekana kukataliwa kwa kishindo, lakini vurugu zilizuka ghafla
kutokana na maamuzi hayo na mkutano ukashindwa kufanikisha zoezi zima la
kuwapata viongozi hao wapya.
Katika hatua nyingine, Juma Haji Duni
alijiengeu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo, baada ya baadhi ya
wajumbe kusisitiza kuwa katiba inamtaka mtu aliyejiuzulu na kuhamia
chama kingine kusubiri miaka miwili ili agombee nafasi ya uongozi ndani
ya chama pale atakaporejea.
Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa CUF,
Shaweji Mketo, alisema kuwa Duni alijiondoa kutokana na maadui wa Ukawa
kutaka kukihujumu chama hicho.
Mkutano huo umeahirishwa hadi utakapotangazwa tena.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment