WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewahimiza wafanyabiashara kuchangamkia fursa ya kuingiza mafuta nchini.
Alisema kwa sasa kampuni zinazojishughulisha na uingizaji mafuta ni chache.
Kutokana na maelezo ya Proesa Muhongo, utekelezaji wa haraka wa hatua
hiyo pamoja na mambo mengine, utaongeza ushindani wa kibiashara na
hatimaye kusaidia kupunguza bei ya bidhaa hiyo hapa nchini.
Alitoa ushauri huo jana wakati wa ziara yake jijini hapa
alipotembelea Bohari ya Kampuni ya GBP, inayohusika na upokeaji mafuta
kupitia bandari ya Tanga na kisha kuyasambaza katika mikoa mbalimbali
nchini.
“Bei ya mafuta yanayouzwa nchini imekua ghali ikilinganishwa na nchi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GBP, Badar Masoud, akitoa
taarifa kwa Waziri Muhongo alisema, uamuzi wa serikali kupitisha shehena
ya mafuta katika bandari ya Tanga umerahisisha upatikanaji wa bidhaa
hiyo na kuondoa adha ya msongamano kwa baadhi ya wasafirishaji
wanaolazimika kwenda Dar es Salaam ili kuyapakia.
“Ombi langu kwako ni kuwa serikali ipange bei elekezi ya kuuza bidhaa
hii hasa kwa mikoa yote ambayo inaunda Kanda ya Kaskazini ili kuleta
usawa sokoni,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment