MAHAK AMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imewahukumu watu wanne
wakiwemo ndugu wawili kutumikia kifungo cha miaka 60 jela baada ya
kupatikana na hatia ya kukamatwa na vipande 25 ya meno ya tembo vyenye
uzito wa kilo 46 vikiwa na thamani ya Sh 371,600,000.
Ndugu hao wawili ni Boniphace Hoza (40) na Elias Hoza (46) wote
wakazi wa Kijiji cha Kalela wilayani Kasulu katika Mkoa wa Kigoma.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Makazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa
baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa
mashitaka ambao haukitia shaka yoyote.
Akitoa hukumu hiyo, Ntengwa aliwahukumu mkazi wa Kijiji cha Ivungwe
katika makazi ya wakimbizi ya Katumba wilayani Mpanda, Justine Baruti
(39) na mkazi wa kijiji cha Kalela, Boniphace Hoza kutumikia kifungo cha
miaka 25 kila mmoja.
Wakati watuhumiwa wengine, kaka wa Boniface, Elias Hoza na Credo
Gervas (45) mkazi wa kijiji cha Ndurumo, Katumba wamehumiwa kila mmoja
kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Mahakama hiyo ilimwachia huru mshitakiwa wa tano, Sadock Masamba
baada ya upande wa mashitaka kushindwa kutoa ushahidi wa kumtia hatiani
mshitakiwa huyo.
Upande wa mashitaka uliongozwa na Wakili wa Serikali wa Mkoa wa
Katavi, Wakyo Simon uliita mashahidi 15 na washitakiwa walitetewa na
Wakili Elias Kifunda na hawakuwa na mashahidi wowote.
Awali, Mwendesha Mashitaka, Mwanasheria wa Serikali Wakyo alidai
mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Desemba 24,
2014 katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani katika Mtaa wa Mji
Mwema, Manispaa ya Mpanda.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, askari wa Hifadhi ya Taifa ya
Katavi na Polisi walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa washitakiwa
hao wamepanga kusafirisha nyara hizo za serikali kutoka mjini Mpanda
hadi mkoani Kigoma kwa basi la abiria la Adventure Connection.
Iliendelea kudaiwa kuwa kutokana taarifa hizo askari wa Tanapa na
Polisi walifika kwenye eneo la tukio na kuwakamata washitakiwa wakiwa na
vipande 46 vya meno ya tembo ndani ya basi hilo la abiria.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa wa kwanza, Baruti siku hiyo alikamatwa na
vipande 18 vyenye uzito wa kilo 33 vyenye thamani ya Sh milioni 49.6 na
mshitakiwa wa pili Boniphace alikamatwa na vipande saba vya uzito wa
kilo 13 na thamani ya Sh milioni 124 wakiwa wamevipakia kwenye basi la
Kampuni ya Adventure Connection.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment