Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN
amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa
kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa
ukadiriaji majengo nchini.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ametoa
kauli hiyo 18-Aug-16 wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji
majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais amesisitiza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa
kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya
kati kwa kiwango cha kisasa (Standard gauge) na ujenzi wa bomba la
mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga, Tanzania na suala la kuhamia
Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga
vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama
nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.
Amesema
serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni
muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi
zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.
Makamu wa Rais SAMIA
SULUHU HASSAN amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania
na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi
zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.
Kwa
upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa MAKAME
MBARAWA amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali
inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi
hivyo na sio vinginevyo.
Home
News
Slider
SAMIA awataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment