MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), amekamatwa na
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa
hadhara jimboni kwake.
Akithibitisha kukamatwa kwake jana jioni, alisema kuwa baada ya
kuhutubia mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Ikungi, alifutwa na
Ofisa wa Polisi na kumwalifu kuwa anahitajika polisi kwa mahojiano.
“Ninawaandikieni maneno haya nikiwa chini ya ulinzi wa polisi
Singida. Nimemaliza kuhutubia mkutano wa hadhara mji mdogo wa Ikungi
ambao ni makao makuu ya Jimbo langu la Singida Mashariki.
“ Mara baada ya kushuka jukwaani nimefuatwa Regional Crimes Officer
wa Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Babu Mollel na
kunitaarifu kuwa ameelekezwa na Regional Police Commander Singida
nikamatwe. Apparently kuna amri ya kunikamata iliyotoka Dar es Salaam.
“Kwa hiyo niko nguvuni na ninasubiri maelekezo ya RPC juu ya
wanakotakiwa kunipeleka. It’s likely nitasafirishwa Dar usiku huu
(jana). In fact ni usiku huu kwa taarifa za sasa hivi. Nitapambana
kutetea haki yetu ya kuwasema watawala popote nitakapokuwa,sitakubali
kunyamazishwa Aluta continua,” alisema Tundu Lissu katika ujumbe wake
uliombazwa jana jioni
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment