Waziri
wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu afahamisha kuwa Uturuki na
Urusi ipo katika mstari mmoja kuhusiana na suluhisho la kisiasa la
mzozo wa Syria pamoja na msaada kwa raia wa Syria.
Cavusoglu katika
maelezo yake alisema kuwa serikali zote mbili za Uturuki na Urusi
hazingependa kuona kuendelea kwa mauaji ya raia wasio na hatia Syria,na
pia hawaoni sawa Aleppo kukabiliwa na mashambulizi mara kwa mara .
Aidha
Cavusoglu alifahamisha kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili
pamoja na jeshi wakishirikiana na idara ya upelelezi watashirikiana
katika shughuli za usalama .
Cavusoglu alisema pia watafanya
ushirikiano na Urusi katika sekta ya Ulinzi hasa ikiwa pia Uturuki ni
mojawapo ya nchi ambazo ni mwanachama wa NATO.
Kuhusu suala la
kuangushwa kwa ndege ya kivita ya Urusi mnamo Novemba 24 mwaka
jana,waziri huyo alifahamisha kuwa wahusika wa kitendo hicho tayari
wamekamatwa na wanaendelea kuulizwa maswali kuhusiana na suala hilo.
Alisema kuwa hiyo ilikuwa mojawapo ya mipango ya kundi l FETO katika juhudi za kuharibu uhusiano baina ya Uturuki na Urusi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


0 comments:
Post a Comment