Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (katikati) akizungumza na Balozi wa Israeli nchini,
Yahel Vilan (kulia) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Israel na
Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Mwigulu,
jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Israeli
nchini, Yahel Vilan alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali ya
ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika
katika ofisi ya Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati)
akimkaribisha Balozi wa Israeli nchini, Yahel Vilan (kushoto), ofisini
kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali
ya ushirikiano kati Israel na Tanzania. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment