Image
Image

13 wafa ajali ya Super Shem na Hiace Mwanza.


Watu 13 wanarifiwa kufa na wengine ambao idadi yao haijafahamika mara moja kujeruhiwa mara baada ya Basi la Super Shem linalofanya safari zake kutoka  Mwanza kwenda Mbeya kuigonga Hiace kwa nyuma katika kijiji cha Hungumalwa Mwanza.
Ajali hiyo imetokea hivi leo Mwendo wa 12:30 alfajiri, hali ambayo imesababisha huzuni kubwa miongoni mwa walioshuhudia sambamba na watanzania mbalimbali waliopata taarifa za tukio hili huku maswali yakiwa mengi juu ya nini sababu za kutokea kwa ajali hiyo ambapo bado Polisi hawajaweka wazi nini kilisababisha mpaka hatua hiyo.
Mashuhuda wa ajali wanadai kuwa mwendo wa haraka na kasi ndio chanzo kilicho sababisha watu 13 kufa katika ajali hiyo,kutokana na Basi la Super Shem kuigonga Hiace hiyo ambapo wanadai asilimia kubwa kwa waliokufa ni abiria waliokuwamo ndani ya Hiace hiyo,kutoka na na kugongwa na kuharibika vibaya mno.

POLISI YATHIBITISHA.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea ajali hiyo na kusema imetokea saa 12:15 asubuhi na ilihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T368 CWQ lililokuwa likotokea kijiji cha Shirima kwenda Mwanza mjini na basi aina ya Scania lenye namba za usajili T874 CWE.
Msangi amesema ajali hiyo ilitokea wakati gari hilo dogo likiingia katika barabara kuu na kugongana na basi lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Mwanza na kusababisha vifo na majeruhi waliokuwa katika gari dogo.
“Nipo njiani naenda eneo la tukio lakini taarifa za awali nilizopokea ni kuwa watu 13 wamefariki duniani na wengine 11 wamejeruhiwa na kati ya hao marehemu wawili ni watoto wadogo, na ajali imetokea katika makutano ya barabara kuu na hiyo kutokea kijiji cha Shirima ilipokuwa ikitokea gari ndogo."
Tukio hili la ajali ya  Super Shem la leo 21 Septemba 2016, linavuta hisia miongoni mwa watanzania  ikiwa ni siku moja tu itokee ajali nyingine basi la Kampuni ya New Force iliyotokea jana tarehe 19 Septemba, 2016 majira ya saa 2:00 Usiku katika Kijiji cha Lilombwi, Kata ya Kifanya, Tarafa ya Igominyi Mkoani Njombe ambapo watu 12 walipoteza maisha na wengine 28 kujeruhiwa.
Mmoja wa majeruhi wa ajali kwenye ajali ya basi la New Force alisema chanzo cha ajili hiyo kilisababishwa na mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa.

Mwenyezi Mungu zilaze panapo stahili kwa waliokufa kutokana na ajali hizi.
Madereva endesheni kwa kuzingatia sheria.
Msipoteze Maisha yawasiokuwa na hatia kwa uzembe wa kukizoea chombo cha moto. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment