MKUU wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera, amesema wakati
umefika kwa Serikali kutunga sheria na adhabu ngumu kwa watu
watakaobainika kufanya vitendo vya kijangili.
Homera aliyasema hayo juzi wakati akitoa salamu za wilaya hiyo pamoja
na changamoto zinazowakabili wakazi wanaoishi karibu na maeneo ya
mapori ya hifadhi kama Selous, kwenye maadhimisho ya siku ya tembo
kitaifa yaliyofanyika wilayani hapa.
Maadhimisho hayo yaliandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
kushirikiana na Shirika la Utunzaji wa Mazingira Duniani (WWF).
Homera alisema majangili wamekuwa wakifanya vitendo haramu kwenye
mapori hayo kwa kuwaua wanyama hasa tembo kwa masilahi yao, hivyo wakati
umefika kwa Serikali kutunga sheria ngumu pamoja na kuweka adhabu
itakayosaidia kuwaokoa wanyama hao wasiendelee kuteketea.
Mkuu huyo akitoa salamu za wilaya hiyo, alisema licha ya Serikali
kufikiria namna ya kutunga sheria hiyo, lakini bado Wizara husika ya
Maliasili na Utalii pamoja na WWF wakae meza moja na kuangalia namna
bora ya kudhibiti wanyama waliopo kwenye hifadhi ili wasiende kwenye
makazi ya binadamu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment