Kikao
hicho kipya cha mwaka kilizinduliwa na mwenyekiti wa kikao cha 71 cha
Baraza Kuu Peter Thomson. Thomson, balozi wa Fiji kwenye Umoja wa
Mataifa alichaguliwa kushika wadhifa huu na Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa mwezi Juni.
Akihutubia
kwenye ufunguzi wa kikao hicho, Thomson alieleza matatarajio yake kuwa
kikao cha 71 cha Baraza Kuu kitaweza kufanya ajenda ya maendeleo
endelevu ikumbukwe na watu mioyoni na kuigeuza kuwa fursa ya utendaji.
"Tunatakiwa
kuona kuwa watu wengi bado hawajafahamu ipasavyo ajenda ya maendeleo
endelevu ya kuelekea mwaka 2030 na hawajaanza kuchukua hatua zinazolenga
kutimiza malengo 17. Kama malengo hayo yanaweza kutimizwa, itaweza
kutokomeza umaskini na kuwahakikishia binadamu wote maendeleo endelevu"
0 comments:
Post a Comment