Kauli
hiyo ya Bw. Steinmeier aliitoa alipokutana na wenzake wa Latvia,
Lithuania, na Estonia jana huko Riga, Latvia, ambapo walibadilishana
maoni kuhusu usalama na ulinzi wa Ulaya, utekelezaji wa azimio la
mkutano mkuu wa Warsaw wa NATO, na pia uhusiano kati ya NATO na Russia.
Baada ya mkutano huo, Bw. Steinmeier alisema, ingawa msukosuko wa
Ukraine bado haujatatuliwa kikamilifu, lakini ni lazima mazungumzo kati
ya NATO na Russia yadumishwe na kupanuliwa.
Hata
hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Latvia Bw. Edgars Rinkevics alisema
sasa mazingira ya kuanza mazungumzo na Russia si mazuri, na kama
mapambano hayatasimamishwa kote nchini Ukraine, basi hakuna uwezekano wa
kuondoa vikwazo walivyoweka dhidi ya Russia.
0 comments:
Post a Comment