Image
Image

Washukiwa 3 wa ugaidi watiwa mbaroni nchini Ujerumani

Washukiwa 3 wa ugaidi ambao ni raia wa Syria wameripotiwa kukamatwa nchini Ujerumani kwa madai ya kujihusisha na kundi la DAESH.Washukiwa wanadaiwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yaliyoendeshwa mjini Paris nchini Ufaransa na kusababisha vifo vya watu wengi.
Ujerumani imewashtaki washukiwa hao kwa utekelezaji wa mashambulizi ya kigaidi ya Paris ya Novemba 13 yaliyopelekea vifo vya watu 132 na kuingia nchini kinyume cha sheria kwa ajili ya maandalizi ya mashambulizi mengine.
Mmoja wa washukiwa hao anadaiwa kujiunga na kundi la DAESH mjini Rakka mwezi Septemba mwaka 2015 na kupokea mafunzo ya utumiaji silaha na mabomu kwa kipindi kifupi.
Maafisa wa polisi wapatao 200 wa Ujerumani waliendesha operesheni dhidi ya ugaidi na kukagua baadhi ya nyumba katika sehemu 3 za hifadhi za wakimbizi.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere ametoa maelezo na kuarifu kwamba harakati za operesheni hiyo zinalenga kukabiliana na ugaidi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment