Shirika
la kukabiliana na dawa za kusisimua misuli duniani WADA limewashtumu
wadukuzi kutoka Urusi kwa kutoa faili za siri za matibabu za wanariadha
wa Marekani walioshiriki katika michezo ya Olimpiki mjini Rio.
Wanariadha
walioathirika ni pamoja na mchezaji wa tenisi Venus na Serena Williams
pamoja na mchezaji wa mazoezi ya viungo Simone Biles.
Kundi
linalojiita Fancy Bears lilikiri kufanya udukuzi huo kuhusu data ya
Wada.Baada ya ufichuzi huo,Bi Biles alisema kuwa amekuwa akitumia dawa
za kutuliza mtu kuhangaika.
Kundi hilo la udukuzi lilimshutumu kwa kutumia dawa ya kusisimua misuli,lakini akasema kuwa amekuwa akifuata sheria.
Mshindi
huyo wa medali nne katika michezo ya Rio Olimpiki alipata ruhusa ya
kutumia dawa hizo zilizopigwa marufuku na Wada ,shirika la wanamichezo
wa viungo nchini Marekani lilisema katika taarifa.
Home
MICHEZO
Slider
WADA yawashtumu wadukuzi wa Urusi kwa kufichua faili za Serena Williams na Biles.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment