Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 14 Septemba, 2016 amemuapisha
Dkt. Ramadhani Kitwana Dau kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.
Kabla ya kuteuliwa
kuwa Balozi, Dkt. Ramadhan Kitwana Dau alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Mhe. Balozi Dkt. Ramadhani
Kitwana Dau anajaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini
Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amewaapisha
Makatibu Tawala wa Mikoa mitatu aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.
Walioapishwa ni kwanza,
Bw. Eliya Mtinangi Ntandu anayekuwa Katibu Tawala wa kwanza wa Mkoa wa Songwe
ulioanzishwa rasmi Mwezi Februari 2016.
Pili,
Bw. Adoh Stephen Mapunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara.
Bw. Adoh Stephen
Mapunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Benedict Richard Ole Kuyan
ambaye amestaafu.
Tatu,
Bw. Tixon Tuliangine Nzunda anayekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa.
Bw. Tixon
Tuliangine Nzunda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Symthies Emmanuel
Pangisa ambaye amestaafu.
Baada ya
kuapishwa, Mhe. Balozi Ramadhani Kitwana Dau na Makatibu Tawala wote watatu
wamekula Kiapo cha Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kilichoongozwa na
Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda na kushuhudiwa na Rais
Magufuli.
Matukio yote
yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
Salaam
14
Septemba, 2016
0 comments:
Post a Comment