Takriban nchi 50 ziliahidi kutoa hifadhi kwa wakimbizi 360,000 pamoja na kuhakikisha msaada wa kifedha.
Rais
Erdogan alitoa hotuba na kuarifu mchango mkubwa wa Uturuki katika suala
la kusaidia wakimbizi, na kukashifu Umoja wa Ulaya kwa kushindwa
kutimiza ahadi kulingana na mkataba wa Machi 18.
Erdogan
alisema, ‘‘Uturuki imeachwa peke yake katika kipindi hiki kigumu cha
kutatua mzozo wa wakimbizi wa Syria. Sisi hatuwezi kurudi nyuma na
tutaendelea kusaidia wakimbizi licha ya kukosa msaada wa Umoja wa Ulaya
na jumuiya ya kimataifa.’’
Erdogan
pia alilaumu jumuiya ya kimataifa kwa kushindwa kuchangia misaada kwa
ajili ya wakimbizi ambao idadi yao kubwa inajumuisha watoto na wanawake.
Erdogan alisisitiza kwamba mzozo wa wakimbizi hauwezi kupata suluhisho bila kuwepo kwa ushirikiano.
Rais
Obama naye alizungumzia suala la wakimbizi na kutambua umuhimu wa
Uturuki ambayo ni miongoni mwa nchi 10 za kwanza zinazochangia kusaidia
wakimbizi wapatao milioni 65.
Katika
maelezo yake, Obama alitoa wito kwa mataifa kufungua mipaka yao kwa
ajili ya kuwapokea wakimbizi na kutoa hifadhi ili kusaidia kutatua
mzozo.
Obama pia alisema kwamba hatua za kufukuza wakimbizi wa Kiislamu zinaweza kuchangia harakati za kigaidi.
Wakati
huo huo, katibu mkuu wa UN Ban Ki-moon alitoa maelezo na kusema,
‘‘Hakuna yoyote inayoweza kusimama peke yake kwa ajili ya kutatua
mizozo. Tunapaswa kushirikiana pamoja.’’
0 comments:
Post a Comment