Meneja
wa Manchester City Pep Guardiola amejipata katika vita vya maneno na
wakala wa kiungo wa kati Yaya Toure baada ya kukosa kumteua kiungo huyo
katika kikosi cha wachezaji 25 watakaoshiriki katika mechi za klabu
bigwa barani Ulaya katika hatua ya makundi.
Guardiola amesema
hatamteua mchezaji huyo hadi pale wakala wake Dimitry Seluk, atakapoomba
msamaha kwa matamshi aliyotamka kwa vyombo vya habari.
Lakini ajenti huyo amesema katu hatafanya hivyo na badala yake akasisitiza kwamba meneja huyo ndiye afaaye kuomba radhi.
''Kwa
nini ni muombe msamaha Guardiola? Sijui maneno ninayostahili kutamka
kuomba radhi, kwa sababu sijafanya kitu chochote. Iwapo nitajihisi
kuomba radhi, basi nitaomba radhi hiyo, lakini sihisi kufanya hivyo.
Kile Guardiola anachokitaka hakitawezekana,'' alisema Seluk kwenye
runinga ya Sky Sport News.
Amesema meneja huyo amewakosea watu wengi
akigusia mtangulizi wake Manuel Pellegrini na kisha kipa nambari moja wa
Manchester City Joe Hart ambaye alilazimika kuondoka klabu hiyo majira
ya joto baada ya kuachwa nje ya mipango ya Guardiola.
"Ni lazima awaombe radhi Yaya na Hart na Pellegrini. Guardiola anashinda mechi kadha na kuanza kufikiria kwamba yeye ni mfalme."
Seluk amesema mteja wake, Toure ,33, ameshiriki katika mechi moja kati ya mechi nane walizozicheza Manchester City msimu huu.
Guardiola
amesema iwapo Seluk atamuomba msamaha yeye, klabu hiyo na wachezaji wa
timu hiyo hapo ndio Yaya atakuwa na nafasi sawa ya kushiriki katika
michezo yote.
''Sitakubali kama kocha kila ajenti, kwenda kwa vyombo
vya habari kuwasilisha malalamiko yao iwapo mchezaji wake
hajashirikishwa kweye kikosi," Guardiola ameongezea.
Guardiol alikuwa kocha wmkuu Barcelona Toure alipouzwa kwa Manchester City mwaka 2010.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment