Kesi kuhusu madai ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu kwa mwana bondia
Tyson Fury itasikilizwa mwezi Novemba baada ya pigano lake na Wladimir
Klitschko Octoba 29.
Fury alimtwanga Klitschko mwaka jana Novemba na hivyo kutwaa mataji
ya WBA, IBF na WBO ya uzani wa juu lakini mwezi juni akashtakiwa kwa
kutumia madawa na shirika la kupambana na matumizi ya dawa la Uingereza
UKAD.
Usimamishaji wa muda uliokuwa umewekwa dhidi yake umeondolewa huku uchunguzi ukiendelea.
Fury, ambaye atapigana na Klitschko kwenye ulingo wa Manchester
amekanusha kuhusika na matumizi yoyote ya madawa na ametishia kuishataki
Ukad.
Fury alitarajiwa kuhudhuria mkutano wa pamoja na mshindani wake
Klitschko Jumatatu alkini hakuweza kufika kutokana na kuharbika kwa gari
lake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment