Mcheza tenisi Stan Wawrinka, ametwaa taji la mashindano ya wazi ya
Marekani, baada ya kumbwaga mchezaji namba moja kwa ubora duniani, Novak
Djokovic, kwa set 6-7 (1-7) 6-4 7-5 6-3, katika mchezo uliochezewa,
Flushing Meadows, New York.
Djokovic raia wa Uswisi alipambana katika hatua za mwanzo, lakini
akawa na uchovu kwenye raundi ya nne, na kujikuta akipoteza mchezo.
Taji hilo ni la kwanza kwa Wawrinka katika US Open, na ni la tatu
kwake katika mataji makubwa ya tenesi (Grand Slam), baada ya kutwaa
mataji ya wazi ya Australia, mwaka 2014, na taji la wazi la Ufaransa
mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment