Image
Image

Marekani yathibitisha kuuawa kwa msemaji wa kundi la DAESH Abu Muhammed Al-Adnani.

                   Msemaji wa kundi la DAESH Abu Muhammed Al-Adnani
Marekani yathibitisha kuuawa kwa msemaji wa kundi la DAESH Abu Muhammed Al-AdnaniIdara ya ulinzi ya Marekani imetoa maelezo na kuthibitisha kuuawa kwa msemaji wa kundi la kigaidi la DAESH Abu Muhammed Al-Adnani katika mji wa Aleppo nchini Syria.
Maelezo yaliyotolewa na idara ya ulinzi yanaarifu kwamba msemaji huyo wa DAESH aliuawa kwenye operesheni ya angani iliyotekelezwa na jeshi la Marekani tarehe 30 Agosti nchini Syria.
Jeshi la Marekani lilifanikiwa kumlenga Al-Adnani kwenye mashambulizi ya angani.
Kwa upande mwingine wizara ya ulinzi ya Urusi ilitoa maelezo tarehe 31 Agosti na kutangaza kumuua msemaji wa DAESH kwenye operesheni iliyotekelezwa na jeshi lake.
Al-Adnani ambaye anatambulika kuwa na uhusiano wa karibu na kiongozi wa DAESH Abubakar Al-Baghdadi, alikuwa ni mmoja wa maafisa wakuu wa kundi hilo.
Mnamo mwaka 2015, Marekani iliwahi kutangaza zawadi ya fedha dola milioni 5 kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa Al-Adnani.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment