Katibu wa baraza kuu la usalama
wa taifa la Iran Bw. Ali Shamkhani amesema jeshi la Marekani linapaswa
kuondoka kutoka Ghuba ya Uajemi kwa sababu uwepo wake kwenye bahari ya
kusini ya Iran unakosa msingi wa kisheria.
Bw. Shamkhani ameongeza kuwa uwepo wa jeshi la Marekani kwenye
Ghuba hiyo ni kinyume na matakwa ya nchi za kanda hiyo, na kusisitiza
kuwa, madai ya Marekani kuwa meli za Iran zinasogelea kwa karibu meli za
kivita za Marekani kwenye Mlango bahari wa Hormuz hayana ukweli wowote.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment