Sergio Aguero ametupia wavuni magoli
matatu yaani hat-trick ya kwanza kwa msimu huu wakati Manchester City
ikiwachachafya Borussia Monchengladbach kwa magoli 4-0 katika mchezo
wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo wa kwanza kwa Pep
Guardiola katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Manchester City,
Aguero aliunganisha krosi ya Aleksandar Kolarov na kuandika goli la
kwanza na kisha kuongeza la pili kwa penati baada ya Ilkay Gundogan
kuchezewa rafu.
Kama hiyo haitoshi Aguero alipachika
goli lake la tatu mbele ya mashabiki 32,000, katika mchezo huo ambao
ulihairishwa kufanyika jumanne kutokana na mvua kubwa. Kelechi
Iheanacho akitokea benchi alifunga goli la nne kwa shuti la umbali wa
yadi 12.
0 comments:
Post a Comment