Image
Image

Kilimanjaro Queens yaibana mbavu Rwanda kwa magoli 3-2 Uganda.


Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, jana ilianza vyema mashindano ya Kombe la Chalenji baada ya kuifunga Rwanda kwa magoli 3-2 katika mchezo uliofanyija Jinja, Uganda.
Katika mchezo huo Kilimanjaro Queens waliandika goli la kwanza katika dakika ya 11 kupitia kwa Asha Rashid na kisha baadaye ilifunga la pili katika dakika ya 28 mfungaji akiwa ni Stumai Abdallah.
Rwanda walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Ibangarrye Marie, na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Kilimanjaro Queens walikuwa mbele kwa mabao 2-1. Katika kipindi cha pili, Kilimanjaro walijifunga kwa goli la Amona Ally na matokeo kuwa 2-2.
Rashid alifunga bao lake la pili na kuiwezesha Kilimanjaro Queens kupata goli la tatu katika dakika ya 65.
Katika mechi za ufunguzi juzi, wenyeji Uganda walitoa kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Kenya, huku Zanzibar ikipokea kichapo cha mbwa mwizi kutoka kwa Burundi baada ya kufungwa magoli 10-0 katika mchezo mwingine wa Kundi A.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment