MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (Nida)
imesema itaanza kutoka vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini kwa
wananchi wote waliokamilisha taratibu za usajili, utambuzi na
kuchukuliwa alama za kibaiolojia kesho ambavyo vitatumika sambamba na
vya zamani.
Taarifa
iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida, Andrew Massawe,
ilieleza kuwa kazi ya ugawaji vitambulisho hivyo itafanyika katika ofisi
zote za Nida zikiwamo ofisi za wilaya zilizoanza usajili, Zanzibar na
mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha,
Kilimanjaro na Ruvuma.
“Waombaji wote ambao vitambulisho vyao viko tayari watatumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (sms) katika simu zao za kiganjani kufahamishwa kufika katika vituo vya Usajili kuchukua vitambulisho vyao,” alieleza Massawe katika taarifa yake hiyo.

0 comments:
Post a Comment