Image
Image

Kundi moja la wafungwa lawavamia walinzi na kuzusha ghasia ndani ya gereza moja nchini Ufaransa.

Kundi moja la wafungwa limeripotiwa kuvamia walinzi na kuzusha ghasia ndani ya gereza moja lililoko tarafa ya Vienne mjini Poitiers nchini Ufaransa.Wafungwa hao waliwavamia walinzi na kutaka kuiba funguo za milango.
Moto mkubwa pia ulizuka na ghasia kuibuka ndani gerezani baada ya tukio hilo.
Vikosi vya usalama vilitumwa katika eneo la tukio na kukabiliana na hali hiyo tete hadi usiku.
Moto huo uliozuka pia uliweza kukabiliwa na timu ya wazima moto.
Wafungwa pamoja na walinzi waliathirika kwa moshi mkubwa uliosababishwa na moto huo.
Wafungwa waliohusika na uvamizi na uzushaji ghasia gerezani wameripotiwa kutiwa mbaroni.
Gereza hilo la Vienna linasemekana kuwa na jumla ya wafungwa 219.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment