Leicester City wamesherehekea ushindi wao wa kwanza wakicheza mara ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata ushindi wa kishindo wa magoli 3-0 dhidi ya klabu ya Brugge, ya Ubelgiji.
Marc Albrighton aliifungia goli la
kwanza Leicester City kwa shuti kufuatia makosa ya beki wa kulia Luis
Hernandez, na kisha baadaye Riyad Mahrez alifunga la pili kwa mpira
wa adhabu alioupiga kwa kuzungusha.
Alikuwa Riyad Mahrez aliyepachika
tena goli la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya mshambuliaji Jamie
Vardy kuangushwa katika eneo la hatari na golikipa.
0 comments:
Post a Comment