Mapema
hivi leo Kumeibuka taarifa za kuogofya jamii ambazo zimekuwa
zikisambaa katika mitandao ya kijamii nchini tanzania, hususani kwa njia
ya Whatsapp na Instagram zikidai kwamba muigizaji mkongwe wa filamu
Tanzania, Muhogo Mchungu amefariki dunia.
Taarifa hizi licha ya kuwa
kwamba wasambaza uzushi huu hawajaanza kwa Muigizaji Muhogo mchungu
wamekuwa wakisambaza mara kadhaa taarifa hizo hata kwa viongozi wakubvwa
wa Serikali kuhusu jambo fulani lenye kushtua jamii.
Kwenye mitaa mbali
mbali na Maofisini hivi leo wameshtushwa na Taarifa yenye kudai kuwa
Muigizaji nguli Mzee Muhogo mchungu hatunaye ulimwenguni, huku
waliowengi wakipatwa na bumbuazi ilikuwaje tena, nini kilimpata kitu ambacho kilikuwa na utata kwa kuwa hakuna aliyekuwa na
taarifa kamili kuhusu hili.
Wakati nasi tukitaka kujua ukweli wa
jambo hili kwamba je huenda ni kweli ama uzushi kutokana na msambaza
taarifa za huyu kuzisambaza na hatimaye kufikia wengi kupitia mitandao
ya kijamii, Baada ya muda kupitia mtandao wake wa Instagram, mwigizaji
wa Bongomovie Batuli amekanusha taarifa hizo na kuandika maneno haya.
Batuli aliandika hivi…
”Muogopeni
Mungu Nyie Mnaozusha Habari Za Vifo Kwa Watu Maarufu,, Mkumbuke Hakuna
Atakayepaa Sote Njia Yetu Ni Moja, Tumieni Mitandao Vizuri Sio Sifa Wala
Ujanja Kutengeneza Habari Zenye Uzushi Kila Baada Ya Muda Fulani, Kifo Ni Cha Wote Hakikimbiliki Mtambue Ipo Siku Na Nyie Mabingwa Wa Kuzusha Kitawatembelea Tu #MunguAnawaona#MolaAkupeMaishaMarefuBaba”
Chonde chonde tujifunze kuandika taarifa zenye ukweli wa mambo kuliko kugushi taarifa zenye kuogofya jamii na familia, yafaa sheria ya mtandao ikaze kamba kwa wazushi wa taarifa ovu kwa taifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment