WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema
hali halisi ya upatikanaji wa dawa katika Bohari ya Dawa nchini (MSD) ni
sawa na asilimia 53, kwani kati ya dawa muhimu 135 zinazohitajika, zipo
aina 71 ghalani.
Pia alisema hali ya upatikanaji wa chanjo nchini utaimarika zaidi kuanzia Oktoba 2, mwaka huu baada ya kupokea shehena mpya.
Katibu mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya alisema juzi
alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyotolewa na taasisi isiyo
ya kiserikali inayofuatilia masuala ya afya, Sikika kuwa MSD inakabiliwa
na upungufu wa dawa na kutoa takwimu kuwa kuna makopo 173 tu ya dawa
aina ya paracetamol nchini.
Dk Ulisubisya alisema hali ya upatikanaji wa dawa itaimarika zaidi
Oktoba mwaka huu hasa kutokana na bohari ya dawa kutumia mikataba ya
muda mrefu na washitiri ili kuimarisha upatikanaji wa dawa wa haraka,
pindi zinapohitajika kulingana na fedha zilizopatikana.
Kwa mujibu wa Dk Ulisubisya, wizara kupitia MSD tayari imepokea
makopo 10,000 ya vidonge vya paracetamol ambayo yameshasambazwa kwenye
vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Pia mkataba kati ya MSD na mtengenezaji wa ndani wenye makopo mengine
138,000 ya vidonge vya paracetamol yenye ujazo wa vidonge 1,000
umekamilika, ambapo dawa hizo zinategemewa kuanza kupokewa kuanzia wiki
ya kwanza ya mwezi wa Oktoba 2016.
Aidha dawa nyingine zilizokuwa zinahitajika zaidi ambazo ni
antibiotics na dawa za kupunguza maumivu, ciprofloxacin, ceftriaxone,
diclofenac, co-trimoxazole, amoxycyline, doxycycline na metronidazole
ziliwasili makao makuu ya MSD, tayari zimeshapelekwa kwenye kanda zote
za MSD tayari kwa kusambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Sako Mwakalobo amesema serikali imewalipa Sh bilioni 20 mpaka sasa, bado wanadai Sh bilioni 142.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment