Image
Image

Mwenyekiti TATOA afunguka utekwaji wa Madereva wa Tanzania na Kenya na magari yao kuchomwa moto,Kongo.


Baada ya kuwepo taarifa za kutekwa nyara kwa Magari ya Mizigo ya Tanzania pamoja na madereva wake sambamba na kuchomwa moto na waasi wa Mai Mai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mwenyekiti wa TATOA, Angelina Ngalula amezungumzia suala hilo kwa kina.
Amesema kuwa watekaji waliteka Magari 12,kati ya hayo 8 ya Tanzania na ma nne ni ya kenya,ambapo baada ya waasi hao kufanya shughuli hiyo waliwapeleka Porini madereva wote wa Malori, ambapo madereva wawili wa Tanzania walifanikiwa kutoroka na hivyo kufanikisha kutoa taarifa za kutekwa.
Taarifa zilidai kuwa waasi hao wanadai dola za Kimarekani elfu nne (karibu shilingi za Kitanzania milioni tisa) kwa kila dereva ama sivyo watawapiga risasi madereva wote. 

 Taarifa Nzima ipo hapa PLay Video(Sauti). 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment