Na Mwandishi Wetu
Shirikisho
la Vyuo vya Elimu ya Juu, limetoa pole kwa wale wote waliokumbwa na
kuathirika na maafa ya janga la tetemeko la ardhi yaliyotokea katika
mkoa wa Kagera, na baadhi ya sehemu za mikoa ya mwanza na Shinyanga.
Pamoja
na pole hizo, Shirikisho hilo, limempongeza Rais John Magufuli na
Serikali yake kwa jumla, kwa kuchukua hatua za haraka kwa kuonyesha
utayari na uharaka katika kuwasaidia walioathirika na janga hilo.
"Tungependa
kumpongeza kipekee, Mheshimiwa Rais kwa kuguswa na jambo hil, kiasi cha
kuamua kuahirisha ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchi Zambia,
ikiwemo kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa Nchi hiyo", .
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na
Mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya
Juu, Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda.
Amesema, pia Shirkisho
linawapongeza wadau na watanzania wote kwa jumla waliojitokeza kwa
haraka na wanaoendelea kujitokea hadi sasa kusaidia kwa namna mbalimbali
wanachi walioathiriwa na janga hilo la tetemeko la ardhi, lililotokea
Septemba 10, mwaka huu.
Zenda amesema Shirikisho pia linatoa rai kwa
wanasiasa kuacha kulitumia janga hilo la tetemeko la ardhi kama fursa
ya kujijenga na kutafuta umaarufu wa kisiasa.
"Shirikisho linawataka
wanasiasa wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa
NCCR Mageuzi James Mbatia kuacha kutumia janga hilo kuchonganisha
wananchi na serkali yao ambayo imeshaanza kuchukua hatua za muda mfupi
na mrefu ikiwemo kuhakikisha waathirika wanapata makazi, chakula na mali
walizopoteza kutokana na janga hilo", alisema Zenda.
Zenda ametoa
mwito kwa walioathirika kuendelea kuwa na shubira kwa kuwa serikali
imeshaanza na inaendelea kuwa karibu nao katika kuhakikisha hali yao
inarejea katika mazingira bora kufuatia janga hilo ambalo lilikuwa la
dharura.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment