Aliyekuwa
kiongozi wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco
Ntaganda ameanza kula baada ya kugoma kwa takriban wiki mbili katika
kizuizi chake kwenye mahakama ya kimataifa ya uhaini huko Hague, Shirika
la AFP linaripoti..
Anakakabiliwa na kesi ya uhalifu wa kivita.
Amepewa
jina la utani "The Terminator" kutokana na shughuli zake Congo,
Ntaganda aligoma kula kulalamika dhidi ya hali inayomkabili kizuizini,
ikiwemo kuhusu suala la kutembelewa na familia yake.
AFP imemnukuu wakili wake Stephane Bourgon aliyesema kwamba ameanza tena kula.
Ameongeza:
''Iwapo
kila kitu kitakwenda sawa, mkewe atafika The Hague kuanzia Alhamisi na
ataweza kumuona bwana Ntaganda kwa kiwango fulani cha faragha,
kitakachokidhi matarajio yake."
Mwaka jana, Ntaganda alikana mashtaka
18 yanayomkabili - ikiwemo mauaji, kuwasijili watoto katika jeshi na
kuwatumia wanawake kama watumwa wa ngono.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment