Wahudumu
4 wa afya na waasi 9 wameuawa karibu na Aleppo wakati makombora ya
angani yalipofyetuliwa usiku na ndege za kivita za Syria na Urusi
shirika la uangalizi la haki za binaadamu Syria limesema Jumatano.
Inafahamika kwamba makombora yameulenga mji wa Khan Touman, unaodhibitwana waasi kusini magharibi mwa Aleppo.
Wahudumu
hao wa afya wanayafanyia kazi mashirika ya usaidizi ya Union of Medical
Care na Relief Organizations, yaliothibitisha vifo hivyo.
Inadhaniwa kuwa maafisa hao wa afya waliitwa katika zahanati moja kuwachukuwa wagonjwa kadhaa kwa matibabu maalum.
Zahanati hiyo imeharibiwa kabisaa, na inahofiwa kuwa kuna watu zaidi waliouawa au kuzikwa chini ya vifusi.
Waasi
hao 9 wa kutoka Jaish al Fatah - kundi la wanamgambo wa kiislamu ambayo
siyo sehemu rasmi ya muungano unaoungwa mkono na mataifa ya magharibi,
lakini ni kitengo kinachohudhumu sambamba na jeshi linalopigania uhuru
wa Syria.
Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulio hilo, lakini
kundi la waasi limelengwa na ndege za kivita za Syria na Urusi katika
siku za nyuma.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment