Shirika lisilo la kiserikali PEC lenye makao makuu yake mjini Geneva
limesema, tangu mwaka huu uanze, zaidi ya waandishi wa habari 95
wameuawa katika nchi 25.
Katika barua ya wazi kwa Kikao cha 33 cha Baraza la haki za binadamu
la Umoja wa Mataifa kinachoendelea, PEC imesema usalama na ulinzi wa
waandishi wa habari unaendelea kuwa mbaya katika nchi zenye vita kama
vile Syria, Yemen, Iraq, Afghanistan na Libya. Barua hiyo imesema kuwa,
lengo la mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari yaliyofanywa na
makundi ya kigaidi na makundi mengine ni kuzuia upatikanaji wa ushahidi
wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
PEC imelihimiza Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa
kufanya uchunguzi wa kina zaidi kuhusu mauaji hao, ikisema kuwa hatua
mpya zinahitajika ili kuboresha hali hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment