Mabingwa watetezi Real Madrid wametikisa nyavu mara mbili katika dakika mbili za mwisho wakitokea nyuma na kuibuka na ushindi wa wa magoli 2-1 Sporting Lisbon katika mchezo wao wa mwanzo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Sporting Lisbon iliongoza kupitia
shuti la chini la Bruno Cesar lakini Cristiano Ronaldo alisawazisha
katika dakika 89 kwa shuti kali la mpira wa adhabu, na kisha baadaye
Alvaro Morata akafunga la pili kwa kichwa.
Katika michezo mingine ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya timu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani ilitoa kipigo
kikali cha magoli 6-0 dhidi ya Legia War, huku Juventus ikitoka sare
ya 0-0 na Sevilla.
0 comments:
Post a Comment