KOCHA wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Boniface Mkwasa ametaja
sababu sita za timu hiyo kufungashiwa virago katika michuano ya kuwania
tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika mwakani Gabon.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) Dar es Salaam jana, Mkwasa alisema moja ya sababu hizo
ni kutofuatwa kwa programU zake kwa madai hakukuwa na fedha.
Stars ilikamilisha ratiba ya michuano hiyo kwa kipigo cha bao 1-0 na
Nigeria katika mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita. Nigeria
pia imekosa nafasi.
Maandalizi ya kuunga unga
“Maandalizi ya kuunga unga, kuna saa nyingine unaandaa programu
ukipeleka kwa mabosi TFF wanakwambia hakuna pesa, wakati mwingine
unapewa sababu wachezaji wapo kwenye majukumu ya timu zao, maandalizi ni
kuunga unga hakuna maandalizi ya kutosha kuleta ushindani”.
Klabu nazo tatizo/wachezaji lege lege Kocha huyo aliwaambia waandishi
wa habari kuwa klabu zinatakiwa kuwaandaa wachezaji wao vizuri ili
wakiitwa kwenye timu ya Taifa wawe na mchango mkubwa wa kuisaidia nchi.
“Timu ya Taifa inategemea wachezaji kutoka kwenye klabu kwa hiyo kama
hawataandaliwa vizuri usitarajie kuwa na timu bora ya kiushindani,”
alisema Mkwasa.
“Wachezaji wetu hawana pumzi, wapo lege lege. Ukiangalia mchezo ule
(dhidi ya Nigeria) dakika ya 60 tu tumeshaishiwa nguvu hii maana yake
wachezaji walikuwa lege lege hawana uwezo wa kucheza dakika 90… “Presha
ilikuwa kubwa sana kipindi cha pili, wachezaji wangu walipoteza umakini
kutokana na kuchoka wakaruhusu goli… “Bado tunahitaji kupata muda mzuri
wa maandalizi ya timu na pia kumtumia vizuri Samatta (Mbwana anayecheza
Genk,Ugiriki) kwenye mechi kama hii. Samatta ni nahodha anakuwa na
jukumu kubwa la kutafuta mpira kuliko kufunga…
“Tutumie msuli wake kufunga sio kumchosha anakimbia kimbia mara
pembeni mara chini, tunatakiwa tupate muda wa maandalizi ili tupate
combination nzuri, vijana wetu wadogo uzoefu hawana tofauti na Nigeria
wakina Obi Mikel wana uzoefu… “Maandalizi ya kuunga unga, kwa aina ya
wachezaji wetu tunatakiwa kuwapa mazoezi ya nguvu ili wawe fiti, lakini
muda unakuwa mfupi, mwisho wa siku tunashindwa kutoa ushindani kwenye
mashindano kimataifa… “Klabu ambayo inacheza mchezo wa nguvu ambayo
haimpi nafasi mtu kucheza wanashindwa, mfano mchezo kama wa Malawi,
Misri ilitupa shida makocha waboreshe wachezaji wao hasa wazawa ili
kuisaidia timu yetu ya taifa,” alisisitiza.
Wachezaji waende gym
“Tunafanya mazoezi kwa siku mbili tunatakiwa tupate muda, klabu
zinatakiwa zihakikishe wachezaji wanakuwa fiti waende gym wakategeneze
vifua wawe fiti. Ethiopia wailaza Stars benchi Mkwasa alisema TFF
inapaswa kuwaandikia barua shirika la ndege la Ethiopia Airways kwa
kushindwa kuwapa huduma bora wachezaji waliotangulia hadi kufikia kulala
kwenye mabenchi, hali iliyosababisha uchovu kwa wanandinga hao.
Ampa tano Manula
Mkwasa aliwapa tano wachezaji wake vijana, hasa mlinda mlango Aishi
Manula kwa kuonesha kiwango kizuri kwa kuokoa michomo mingi ambayo
angekuwa lege lege Stars ingeambulia magoli zaidi ya sita. Alia na Caf
Mkwasa alisema kitu kingine kilichosababisha Stars kushindwa kusonga
mbele kwenye michuano hiyo ni kupangiwa mechi ngumu dhidi ya nchi ambazo
ziko juu kwenye viwango vya FIFA.
“Angalia tumepangwa kwenye kundi lenye nchi kama Misri na Nigeria
ambazo hazikufuzu michuano hiyo kwa miaka miwili sasa unategemea
ingekuwaje. Halafu mechi zetu nyingi za mwisho tunamalizia ugenini.
“Hata sisi tungepangiwa na Botswana, Namibia tungefurukuta tungeingia
fainali, hao Uganda mnaowashangilia kundi lao lilikuwa dhaifu, TFF
wakikaa kwenye vikao vyao vya CAF huku walisemee hili sisi saizi zetu
Uganda, Rwanda, Kenya wangetupangia hao ndio saizi zetu. rekodi sikujua
kama inawezekana”.
Aidha Mkwasa pia alisema jambo lingine lililomkera ni wachezaji wa
timu hiyo kutumia jezi moja ambapo walilazimika kuivaa kwenye mazoezi na
kwenye mechi. “Ifike mahali tubadilike, wachezaji jezi moja, zinaloa
jasho wanakamua alafu ndio wanavaa kwa mechi, ilipaswa kuwe na jezi
nyingine za kubadilisha hii imekwaza sana wachezaji hata mimi mwenyewe
imeniumiza mno... “Mpira wa kisasa huwezi kuvaa jezi moja tunarudi kule
kule kwa miaka ya nyuma wakati tulishatoka huko.
Atishia kuitosa Stars
Mkwasa alisema yupo njia panda kuendelea kuinoa timu hiyo kwa kile
alichoeleza kuwa ni kuchoshwa na mazingira ambayo si rafiki ya ufanyaji
kazi.
“Mara nyingi ukisema ukweli unaonekana mbaya, ila mimi sijali kuna
vitu ambavyo vinanikwaza sana na kunipa uzito wa kuendelea na kazi
yangu, hata kama watataka niendele kufundisha ni lazima tukae vikao
viwili vitatu tukubaliane na nitekelezewe nitakayohitaji la sivyo
sitakuwa tayari,” alisema Mkwasa.
Sababu nyingine ambayo huenda imechangia Mkwasa kutumbukia nyongo
kuiona timu ya Taifa imeelezwa kuwa ni TFF kukiuka makubaliano yake
katika mkataba ukiwemo kumpa nyumba, usafiri ingawa kocha huyo amekuwa
akijituma na kujikuta akiishia kufanya kazi katika mazingira magumu.
Juni 21 mwaka jana, TFF ilisitisha mkataba na kocha wa kigeni kutoka
Uholanzi, Mart Nooij baada ya Stars kunyukwa mabao 3-0 na Uganda Uganda
(The Cranes) kwenye mechi za kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa
Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) na kumteua Mkwasa kuchukua nafasi
hiyo.
Home
MICHEZO
Slider
Sababu sita za Taifa Stars kufungashiwa virago fainali za Kombe la Mataifa Afrika ziko hapa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment