Serikali
ya Uturuki imelikashifu jarida la Der Spiegel kutoka Ujerumani kwa
muundo wa gamba lake tata linalomchezea shere rais Recep Tayyip Erdogan.
Msemaji
wa wizara ya mambo ya nje nchini Ujerumani Tanju Bilgiç alitoa maelezo
kuhusu tukio hilo na kuarifu kwamba jarida la Der Spiegel pia
limechafulia jina Uislamu kwa muundo wa gamba lake.
Akibainisha
kwamba jarida hilo lilikuwa na lengo la kuchafulia jina Uturuki, Bilgiç
alisema, ''Jarida la Der Spiegel limetengeza muundo wa gamba lake kwa
lengo la kuharibia sifa Uturuki ionekane vibaya barani Ulaya. Na
uharibifu huo si wa Uturuki pekee bali pia ni wa Uislamu kwa ujumla.''
Bilgiç
pia alifahamisha kwamba wananchi wa Uturuki wanapinga harakati zozote
zinazolenga kumkashifu au kumkejeli rais Erdogan aliyechaguliwa kuongoza
nchi kwa njia ya haki na demokrasia.
Jarida
la Der Spiegel lilikuwa limepamba gamba lake kwa picha ya Erdogan
iliyozungukwa na minara ya msikiti iliyobadilishwa na kufanywa kuwa kama
makombora.
Ni
wazi kwamba jarida hilo lilifumbia macho janga la jaribio la mapinduzi
ya Julai 15 ya wahaini wa FETO yaliyoendeshwa kwa lengo la kuvuruga nchi
na demokrasia.
0 comments:
Post a Comment