BAADHI ya majeruhi wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera,
waliopata majeraha makubwa na matatizo ya mifupa, wanaweza kupelekwa Dar
es Salaam katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MOI) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu zaidi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu alisema kuwa wizara imejipanga na kushiriki ipasavyo, hivyo
waathirika wa tetemeko hilo watakaobanika kupata matatizo ya mifupa
itabidi wasafirishwe na kwenda kupatiwa matatibu katika taasisi hiyo.
Ummy alibainisha hayo wakati wa kuhitimishwa mjadala wa Muswada wa
Sheria wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu 2016 na Muswada wa Sheria wa
Usimamizi wa Wataalamu wa Kemia 2016.
Alisema nia ya serikali ni kuona majeruhi wanapata matibabu haraka
ili waweze kupona na kutoa pole kwa watu wote walioathirika na tukio
hilo, lililotokea Septemba 10, mwaka huu mkoani humo na katika mikoa ya
jirani ya Mwanza, Geita na Shinyanga. Hadi Jumanne serikali imesema
jumla ya watu 17 ndio wamekufa kutokana na tetemeko hilo na wengine 252
kujeruhiwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), George Simbachawene alisema hayo wakati alipokuwa anasoma
kauli ya serikali bungeni mjini hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu.
Simbachawene alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tisa alasiri
na ukubwa wake ulikuwa wa kiwango cha 5.7 katika vipimo vya Richter.
Alisema majeruhi waliolazwa katika hospitali mbalimbali za mkoani
humo ni 169, waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani ni 83 ambapo
jumla yao ni majeruhi 252.
Alisema nyumba za makazi zilizoanguka ni 840 na nyumba za makazi
zenye nyufa ni 1,264 wakati majengo ya taasisi yaliyoripotiwa kuanguka
ama kupata nyufa ni 44.
Home
News
Slider
Waliopata majeraha makubwa na matatizo ya mifupa kwenye tetemeko la ardhi kupelekwa MOI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment