Image
Image

6 wafariki, 21 wajeruhiwa kwenye mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa mjini Baghdad

Watu 6 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Baghdad nchini Iraq.Mashambulizi hayo yalitekelezwa kwa kutumia bomu lililotegwa ndani ya gari moja la wakfu wa Sunni na kulipukia katika eneo la Es-Seyyidiyah.
Mashambulizi mengine ya bomu yalitekelezwa katika maeneo ya Iskan, Es-Suleyh na Ed-Dura ambapo watu 5 walipoteza maisha na wengine 21 wakajeruhiwa.
Hakuna yeyote aliyehusishwa na utekelezaji wa mashambulizi hayo.
Hata hivyo kundi la DAESH linashukiwa kuendesha mashambulizi hayo kutokana na harakati zake za kigaidi dhidi ya serikali katika miezi ya hivi karibuni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment