KUNDI la wataalamu wa afya kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, limewasili wilayani Ngorongoro mkoani Arusha
katika Kata ya Pinyinyi, kuchunguza ugonjwa wa kutapika damu ulioua watu
21.
Kuwasili wa wataalamu hao, kumethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Gambo na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Omari Sukari.
Gambo alilieleza gazeti hili kuwa timu hiyo iliwasili kijijini Pinyinyi
wiki iliyopita.
Alisema hajui timu hiyo itakaa siku ngapi kijijini humo kuchunguza
ugonjwa huo, lakini anachojua imeshawasili na imeshaanza kufanya kazi
kwa kuwatafuta wale waliougua na wanaogua ugonjwa huo wa ajabu. Alisema
baada ya kukamilisha uchunguzi wao na kupima kila mwananchi aliyepatwa
ugonjwa huo na kupona, watatoa taarifa rasmi.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Sukari alikiri kufika kwa timu
hiyo, lakini hakuwa tayari kusema chochote kwani yeye sio msemaji wa
kundi hilo la wataalamu.
Kujulikana kwa ugonjwa huo, kulitokana na ziara ya Gambo katika
kijiji hicho na Mtendaji wa kata hiyo, James Mushi katika risala yake
alieleza jinsi ugonjwa huo unavyoua wananchi.
Home
Afya
Slider
Wataalamu wa afya watua Ngorongoro kuchunguza ugonjwa wa kutapika damu ulioua watu 21.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment